
Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Buhigwe, mkoani Kigoma wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania M he.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya..
Ofisi hiyo imefunguliwa jana Oktoba 17, 2022 na Mh Rais Samia ambaye amasema:” Serikali imeamua kuboresha utawala bora kwa kuhakikisha inajenda ofisi na ununuzi wa vitendea kazi ili huduma bora zitolewe kwa wananchi kwa karibu.”
Wananchi hao wamesema hatua hiyo itawasaidia kutatua kero za wananchi kwa kuwa limejengwa karibu na wananchi
Akizungumza leo, Bi.Mary Johson mkazi wa Buhigwe amesema awali jengo la Mkuu wa Wilaya lilikuwa dogo na kukosekana kwa baadhi ya huduma na kusisitiza kwa sasa wananchi watakuwa na uhakika wa kupata huduma muhimu sehemu moja
“Jengo hili la Mkuu wa Wilaya lina ofisi zote muhimu kama uhamiaji, vizazi na vifo, ofisi ya Mbunge, hizi zote zitasaidia kupunguza changamoto iliyokuwepo ya kutembea hadi Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu.”
Naye Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Kanali Michael Masala amesema Serikali imedhamiria kusogeza huduma zake kwa wananchi ambazo zitayolewa kwa ubora.
” Wananchi wanapokuja kupatiwa huduma wakute maeneo ambayo watahudumiwa kwa urahisi na kwa haraka, na huduma zipatikane eneo moja.”
Aidha , Kanal Masala amemshukuru Rais Samia kwa kutoa takribani Sh bilioni 1.337 kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo.

ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT