Uongozi wa klabu ya Yanga umewataarifu mashabiki na Wanachama wake kuwa Nasreddin Nabi, bado ni kocha mkuu wa klabu hiyo
–
Nabi ambaye alijiunga na Yanga SC April, 2021 na amekuwa na rekodi nzuri klabuni hapo akiiongoza kubeba Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita, bila kupoteza.
–
Akizungumza na YANGA MEDIA, Mtendaji Mkuu wa Yanga, Andre Mtine amewaomba mashabiki na wanachama wa Yanga kufatilia taarifa za uhakika za timu yao kupitia vyanzo rasmi vya habari vya klabu.
–
Uongozi unamtakia kila la kheri kocha Nabi na benchi lake la ufundi kwenye maandalizi ya mchezo wa kesho wa Ligi Kuu dhidi ya KMC utakaopigwa saa 1:00 jioni kwenye uwania wa Beniamin Mkapa.