Kocha wa Manchester United, Erik Ten Hag amesema atamalizana na mchezaji wake Cristiano Ronaldo baada ya kuonesha kitendo cha utovu wa nidhamu katika pambano dhidi ya Totenham Hotspurs lililomalizika kwa Manchester United kushinda kwa mabao 2-0.
–
Katika mchezo huo Ronaldo alionekana kuondoka uwanjani na Kwenda kwenye vyumba vya kubadilishia nguo ikiwa ni dakika 10 kabla ya mchezo kumalizika ikiwa ni ishara ya kuonesha kutoridhishwa na kukaa benchi.
Akijibu swali kwa mwandishi wa Habari mara baada ya mchezo kumalizika Ten Hag alinukuliwa akisema“Alikuwepo pale, nilimuona lakini sikuongea naye leo tunasherekea kiwango tulichoonyesha na kupata ushindi nitashughulika naye kesho (leo)