ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Tuesday, March 28, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result
ADVERTISEMENT

ROYAL TOUR NA KUKUZA UTALII NCHINI

Tanzania, Afrika Mashariki

ALFRED MTEWELE by ALFRED MTEWELE
Oct 7, 2022
in HABARI
0
ROYAL TOUR NA KUKUZA UTALII NCHINI
0
SHARES
98
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter
ADVERTISEMENT

May be an image of 3 people and outdoors

ADVERTISEMENT
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema takwimu za mwaka 2021 zinaonesha kuwa watalii wanaokuja nchini Tanzania wameongezeka kwa asilimia 48.6 kutoka watalii 620,867 mwaka 2020 na kufikia watalii 922,692 mwaka 2021.
Mheshimiwa Majaliwa pia mapato yatokanayo na utalii yameongezeka kwa asilimia 81.8 kutoka Dola za Marekani milioni 714.59 mwaka 2020 na kufikia Dola za Marekani bilioni 1.3 mwaka 2021.
Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Oktoba 5, 2022) alipomuwakilisha Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwenye ufunguzi wa Mkutano wa 65 wa Shirika la Utalii Duniani – Kamisheni ya Afrika unaofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Gran Melia Jijini Arusha.
“Pia takwimu za mwaka 2022 zinaonesha kuwa Sekta ya Utalii inazidi kuimarika zaidi hususan baada ya uzinduzi wa Programu Maalumu iliyotekelezwa na Mheshimiwa Rais Samia ya The Roya Tour iliyozinduliwa rasmi Aprili 2022 katika soko letu la utalii la kimkakati nchini Marekani.”
Amesema kuwa mafanikio hayo ni matokeo ya mwongozo mzuri uliotolewa na Shirika la Utalii Duniani kwa nchi wanachama ikiwemo Tanzania katika kukabiliana na athari za UVIKO – 19. “Kwa msingi huo, ninatumia fursa hii kulishukuru Shirika la Utalii Duniani hususan, kwako Mheshimiwa Zurab Pololikashvili, Katibu Mkuu wa Shirika la Utalii Duniani kwa kuiongoza vema sekta ya utalii katika kipindi chote cha janga hilo.”
Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema lengo la Serikali ni kuendelea kuongeza idadi ya watalii wanaoingia nchini hadi kufikia watalii milioni tano na mapato ya Dola za Marekani bilioni sita ifikapo mwaka 2025.”Utajiri wa vivutio vya utalii tulivyonavyo umeifanya sekta ya utalii kuwa muhimili muhimu wa uchumi wa nchi yetu.”
Naye, Katibu Mkuu wa Shirika la Utalii Duniani, Zurab Pololikashvili amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo zina vivutio bora vya kutembelea kwa ajili ya utalii na watu wengi duniani wameitambua kupitia filamu maarufu ya The Royal Tour.
“Wiki iliyopita tulisherehekea siku ya utalii duniani iliyokuwa na kaulimbiu ya Rethinking Tourism, ambayo tunaamini itasaidia kuirejesha sekta hiyo katika hali yake ya kawaida na kuendelea kusaidia kutoa mchango katika ukuaji wa uchumi na kuongeza idadi ya ajira.”
May be an image of 9 people, people sitting, people standing and indoor

RelatedPosts

WAZIRI MCHENGERWA AZINDUA BOTI YA KITALII YA TAWA SEA CRUSIER

WAZIRI MCHENGERWA AZINDUA BOTI YA KITALII YA TAWA SEA CRUSIER

Mar 16, 2023

ANUSURIKA KIFO KISA KUTAKA PIGA SELFIE NA TEMBO

Mar 14, 2023
Load More
ADVERTISEMENT

Related

Tags: WIZARA YA UTALII
ADVERTISEMENT
ALFRED MTEWELE

ALFRED MTEWELE

Related Posts

TAASISI YA GREEN KIDS AND YOUTH FOUNDATION  KUENDELEZA MAHUSIANO BORA NA WADAU KATIKA KUTETEA UNYANYASAJI WA KIJINSIA
HABARI

TAASISI YA GREEN KIDS AND YOUTH FOUNDATION KUENDELEZA MAHUSIANO BORA NA WADAU KATIKA KUTETEA UNYANYASAJI WA KIJINSIA

by Ally Hamis Zingizi
Mar 27, 2023
NALA kuwekeza zaidi ya Sh. Bilioni 2 baada ya kupata leseni ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT)
HABARI

NALA kuwekeza zaidi ya Sh. Bilioni 2 baada ya kupata leseni ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT)

by I am Krantz
Mar 27, 2023
Naibu Waziri   aipongeza Benki ya NBC kwa kusaidia maendeleo ya  michezo
HABARI

Naibu Waziri aipongeza Benki ya NBC kwa kusaidia maendeleo ya michezo

by I am Krantz
Mar 27, 2023
MZEE WA MIAKA 92 AFUNGA NDOA YA TANO MWAKA MMOJA BAADA YA NDOA NNE KUVUNJIKA
HABARI

MZEE WA MIAKA 92 AFUNGA NDOA YA TANO MWAKA MMOJA BAADA YA NDOA NNE KUVUNJIKA

by Shabani Rapwi
Mar 27, 2023
BAKWATA YASHIKILIA MSIMAMO NDOA MIAKA 14
HABARI

BAKWATA YASHIKILIA MSIMAMO NDOA MIAKA 14

by Shabani Rapwi
Mar 27, 2023
MOURINHO KOCHA BORA WA KARNE – ÖZIL
HABARI

MOURINHO KOCHA BORA WA KARNE – ÖZIL

by Shabani Rapwi
Mar 27, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

ADVERTISEMENT
October 2022
M T W T F S S
 12
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930
31  
« Sep   Nov »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In