Denis Onyango kutoka Uganda amechaguliwa kama kipa bora katika Timu ya TotalEnergies Caf Champions League ya muongo [2010-2020] na mashabiki.
–
Katika kura ya maoni iliyoendeshwa kwenye mitandao ya kijamii ya Caf, Onyango ambaye alishinda shindano hilo akiwa na Mamelodi Sundowns mwaka wa 2016 alipata kura nyingi zaidi kati ya walinda mlango wengine.
–
Mchezaji bora wa Afrika wa mwaka 2016 anayetokea Tanzania ni mmoja tu kati ya wachezaji wawili wa Afrika Mashariki kwenye timu hiyo sambamba na nahodha wa Tanzania Mbwana Ally Samatta.
–
Samatta aliyeichezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa zaidi ya miaka mitano pia alishinda shindano hilo kabla ya kutimkia barani Ulaya ambako amewahi kucheza Ubelgiji, Uingereza na Uturuki.
–
Waafrika Kaskazini wanatawala kikosi hicho wakiwa na Wael Gomma, Ahmed Fatty, Hossam Ghaly, Hossam Ashour, Ali Maaloul, na Walid Soliman.
–
Mzambia Stopilla Sunzu ambaye pia aliwahi kuchezea TP Mazembe kabla ya kutimkia Ufaransa anaifanya timu hiyo kuwa kiini cha ulinzi huku Percy Tau, mshindi wa Ligi ya Mabingwa wa Caf akiwa na Sundowns na Al Ahly pamoja na Mzimbabwe Khama Billiat akitengeneza timu hiyo.