Timu ya Wanawake, Simba Queens leo imeingia mkataba wa udhamini wa miaka mitano na kampuni ya michezo ya kubashiri ya M-Bet wenye thamani ya Tsh. bilioni moja.
Ikiwa kampuni hio ilisalia kuwa mdhamini mkuu wa Klabu ya Simba SC ambapo nembo yake huonekana katika jezi za klabu hio sasa itahamia na upande wa Timu ya Wanawake kupitia mkataba huo.
Hivyo hivi karibuni timu ya Simba Queens itaanza kutumia jezi zenye nembo ya M-Bet kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake.



ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT