
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa ameziagiza mamlaka za Serikali za Mitaa kuwashirikisha Wazee kupitia mabaraza yao kushiriki kwenye vikao vya maamuzi kuanzia ngazi za vijiji na mitaa hadi Mabaraza ya Madiwani.
Akizungumza kwa niaba ya Mhe. Majaliwa, Waziri wa Nchi Ofisi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene wakati wa maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Wazee yaliyofanyika Jijini Dodoma Oktoba 03, 2022.
Mhe. Majaliwa amesema Serikali inafanya jitihada mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha Jamii inawatambua na kuwathamini wazee ikiwemo kuanzisha Kampeni ya mpishe Mzee kwenye maeneo mbalimbali ya kutolea Huduma.
“Kila Halmashauri iweke maeneo mazuri ya kukaa wakati wa mikutano ya mabaraza ya Madiwani na Wazee wanapo jadili mambo yao mzingatie Uzalendo na ujenzi wa maadili mema kwa watoto wetu” amesema Simbachawene
Simbachawene amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutambua Makundi muhimu hususani Wazee kwa kuanzisha Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa ajili ya kushughulikia Makundi hayo kwani kabla
Makundi hayo yalikuwa ,yanakosa mahali maalum pa kupeleka Masuala yao .
Ameongeza kwamba, Serikali inaendelea kuelimisha jamii kuzingatia ulinzi na usalama kwa Wazee Kwa kuanzisha mabaraza ya wazee 20749 Kwa lengo la kuwapa fursa ya kujadili mambo yao na kuwa chombo cha kushauri Jamii.
Waziri Simbachawene ametumia nafasi hiyo kutoa Rai kwa viongozi na Wazee kuwa pamoja na kutumia mabaraza hayo kujadili Ustawi wao wahakikisha umoja na Jumuiya nyingine za Wazee zinatambuliwa na kusajiliwa katika maeneo yao na taarifa za utekelezaji wa mabaraza ya Wazee zijumuishwe kwenye kamati za Maendeleo ili mawazo yao yaweze kuzingatiwa na kufanyiwa kazi.
Ametoa wito kwa Jamii kushirikiana kuzuia ukatili kuliko kunyamaza na hatimaye kunung’unuka na kuombolea matukio yanapotokea.
Kwa upande wake Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amesema maadhimisho hayo ni matokeo ya maamuzi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuanzisha Wizara hii.


ADVERTISEMENT