Watu 174 wanahofiwa kupoteza maisha na wengine 180 kujeruhiwa huko nchini Indonesia 🇮🇩 kutokana na kukanyagwa baada ya polisi kurusha mabomu ya machozi ili kutuliza ghasia zilizotokea wakati ya mechi ya Debry iliyochezea katika uwanja wa Kanjuruhan nchini humo na kuifanya kuwa moja ya matukio mabaya zaidi ya michezo duniani.
–
Ghasia zilizuka baada ya mchezo kukamilika jana jioni Jumamosi, Oktoba 1 na wenyeji Arema FC ya East Java’s Malang city kupoteza dhidi ya Persebaya Surabaya kwa kichapo cha 3-2.
–
Baada ya Arema FC kupoteza mchezo huo, maelfu ya wafuasi wa Arema, wajulikanao kama “Aremania” walianza kurusha chupa na vitu vingine kwa wachezaji na maafisa wa soka.
Mashabiki walifurika kwenye uwanja wa Kanjuruhan wakipinga na kuutaka uongozi wa Arema kueleza ni kwa nini baada ya miaka 23 ya michezo ya nyumbani bila kufungwa mechi ile iliisha kwa kupoteza.
–
Ghasia hizo zilienea nje ya uwanja huo ambapo takribani magari matano ya polisi yaliangushwa na kuchomwa moto huku kukiwa na machafuko hayo.
Askari wa kutuliza ghasia walijibu kwa kurusha mabomu ya machozi, ikiwa ni pamoja na kuelekea kwenye viwanja vya uwanja, na kusababisha hofu miongoni mwa umati.