Mkurugenzi wa Idara ya Leseni na Ufuatiliaji TCRA, Bw. John Daffa akifuatiwa na Mkurugenzi wa Masuala ya Kisekta TCRA, Dr. Emmanuel Manasseh (picha inayofuata) wakisaini nyaraka za mwisho za makubaliano ya Nchi wanachama wa Shirika la Mawasiliano Duniani (ITU). Nyaraka hizo zinatokana na kazi ya maandalizi iliyofanywa kwa kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja, pamoja na vikao vya majadiliano vilivyofanyika nchini Romania kwa muda wa wiki tatu. Matokeo ya kazi hii, yameweza kuja na Maazimio, Maamuzi, na Mpango Mkakati wa Shirika kwa kipindi 2024-2027.
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT