Mshambulizi wa Manchester United Cristiano Ronaldo anakabiliwa na faini ya pauni milioni 1 na klabu hiyo baada ya kutoka nje ya ushindi dhidi ya Tottenham. (Star)
United inaweza kumwachilia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 kwenda bure mwezi Januari ikiwa hakuna mtu atakayemsajili. (inews)
Real Madrid, Paris St-Germain na Manchester City wametuma maskauti kumtazama winga wa Napoli na Georgia Khvicha Kvaratskhelia, 21.. (90min)
Chelsea wako tayari kumruhusu mshambuliaji wa Ubelgiji Romelu Lukaku, 29, kusalia kwa mkopo Inter Milan msimu ujao kabla ya kufutilia mbali mamilioni ya pauni kwa kumuuza. (Gazzetta dello Sport, via Mirror)
Crystal Palace wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Blackburn na Chile mwezi Januari Ben Brereton Diaz, 23. (Sun)
Kwengineko, Sevilla wanaongoza Everton, Leeds na Fulham katika mbio za kumsajili Brereton Diaz mwezi Januari (Football Insider)
GETTY IMAGES
Lakini kiungo wa Slovakia Stanislav Lobotka, 27, anatazamiwa kusaini mkataba mpya na Napoli, licha ya kunyatiwa na Arsenal, Liverpool na Tottenham. (90min)
Arsenal walikuwa na nia ya kumsajili beki wa Nigeria Calvin Bassey, 22, kutoka Rangers msimu wa joto – kabla ya kuhamia Ajax. (Own Goal Nigeria)