Kiungo wa kati wa Chelsea na Italia Jorginho, 30, anatafuta nyongeza ya mshahara wa hadi pauni 150,000 kwa wiki kabla ya kusaini mkataba mpya na klabu hiyo. (Evening Standard)
AC Milan wanashinikiza kuharakisha mazungumzo juu ya mkataba mpya na mshambuliaji wa Ureno Rafael Leao mwenye umri wa miaka 23 huku klabu ya Manchester united ikimwinda (Express)

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES
Maelezo ya picha,Milan Skrinier
Mlinzi wa kati wa Inter Milan na Slovakia Milan Skriniar, 27, na Leao wa AC Milan wanaweza kusaini kandarasi mpya na vilabu vyao vya Italia licha ya kunyatiwa na Chelsea. (Evening Standard)
Besiktas wamekanusha uvumi unaoenea mtandaoni kwamba wanalazimika kumchezesha mchezaji aliyecheza kwa mkopo Everton Dele Alli, 26, baada ya kiungo huyo wa kati Muingereza kurejea kutoka jeraha la paja. (Liverpool Echo)
GETTY IMAGES
Maelezo ya picha,Lionel Messi
Kikundi kidogo cha mashabiki wa Barcelona kimeenda mahakamani kuhusu uhamisho wa mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi kwenda Paris St-Germain mwaka wa 2021. Mawakili walifika mbele ya hakimu mkuu katika mahakama ya Ulaya na kuhoji kwamba uhamisho wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35 ulivunja sheria za misaada Ulaya. (Guardian)
Beki wa zamani wa Arsenal William Gallas anasema mshambuliaji wa sasa wa Gunners na Brazil Gabriel Martinelli, 21, bado hajatosha kuhamia Real Madrid. (TalkSPORT)
Wakati huohuo, mkurugenzi wa ufundi wa Gunners Edu anasakwa na vilabu vingine viwili vya Ulaya lakini kiungo huyo wa zamani wa Arsenal “amezingatia 100%” jukumu lake katika kikosi cha London kaskazini. (Fabrizio Romano)
Juventus wanavutiwa na kiungo wa kati wa Atletico Madrid na Argentina Rodrigo De Paul, 28. (Calciomercato – in Italian)
SOURCE; BBC SWAHILI