Liverpool inaongoza kampeni ya kumsajili mchezaji wa Borussia Dortmund mwenye umri wa miaka 17 raia wa Ujerumani Youssoufa Moukoko. (Sport, via Mail)
Arsenal imepumzisha azma yake ya kumsajili mlinzi wa Eintracht Frankfurt raia wa Ufaransa Evan Ndicka, mwenye umri wa miaka 23, baada ya kumkabidhi raia wa Brazil Gabriel Magalhaes mkataba mpya. (Express)
Itaibidi Aston Villa illipe Euro milioni 10 (£8.68m) kumsajili Meneja wa Sporting Lisbon Ruben Amorim kama Meneja wake mpya. (Telegraph)
Aliyekuwa meneja wa Tottenham Tim Sherwood anasema wasiwasi kuhusu mustakabali wa meneja wa sasa Antonio Conte unamzuia mchezaji wa kiungo cha mbele Harry Kane, mwenye umri wa miaka 29, na raia wa Korea Kusini Son Heung-min, aliye na miaka 30, kusaini mikataba mipya. (Sky Sports, via Express)
GETTY IMAGES
Mkurugenzi wa michezo wa Bayern Munich Hasan Salihamidzic anasema Kane ni “mojawapo ya wachezaji bora duniani”. (Talksport)
Huenda Chelsea ikampatia winga raia wa Morocco Hakim Ziyech, mwenye umri wa miaka 29, katika mkataba wa kukabidhi mchezaji na malipo kwa mchezaji wa kiungo cha kati wa Juventus Adrien Rabiot, mwenye umri wa miaka 27. (Calciomercato)
Afisa mkuu mtendaji wa Ajax Edwin van der Sar anasema ameiambia Arsenal kwamba klabu hiyo ya Uholanzi haitomuuza mlinzi wake raia wa Argentina Lisandro Martinez, wiki kadhaa kabla ajiunge na Manchester United. (Times)
Mwamba wa Leicester City Gary Lineker anasema timu hiyo ‘ilijishindia dhahabu’ kwa usajili wa msimu wa joto wa mlinzi rai awa Ubelgiji Wout Faes mwenye umri wa miaka 24 kwa £15m. (Leicestershire Live)