Mkufunzi wa Newcastle United Eddie Howe amekataa kumsajili mshambuliaji wa Manchester United na Ureno Cristiano Ronaldo kwa sababu ya umri wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 37 (90min)
Manchester City haitakumbana na vikwazo vya kifedha katika kumsajili fowadi wa Ufaransa Kylian Mbappe, 23, ambaye anataka kuondoka Paris St-Germain licha ya kusaini mkataba mpya msimu wa joto. (Marca – in Spanish)
Meneja wa England Gareth Southgate anaweza kukusanya bonasi ya pauni milioni 4 ikiwa atawaongoza Three Lions kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia nchini Qatar. (Sun)
AC Milan wanaweza kumnunua kiungo wa kati wa Chelsea na Uingereza Ruben Loftus-Cheek, 26, mwezi Januari. (Calciomercato – in Italian)
Beki wa kati wa Juventus na Italia Leonardo Bonucci, 35, amehusishwa na uhamisho wa kujiunga na Tottenham baada ya kuomba kuuzwa katika dirisha la uhamisho la Januari. (Football Italia)
Chelsea walikuwa wakipanga kumpa beki wa kulia wa England Reece James, 22, na kiungo wa kati Mason Mount 23, mikataba mipya ya muda mrefu na klabu hiyo, hata kabla ya kuuzwa kwa timu hiyo kwa kundi la makapuni ya mwekezaji Mmarekani Todd Boehly mwezi Mei.. (CBS Sports)
Beki wa Liverpool na Uholanzi Virgil van Dijk, 31, anasema kuondoka kwa fowadi wa Senegal Sadio Mane, 30, kwenda Bayern Munich sio sababu ya wao kunaza vibaya katika msimu huu wa Ligi ya Premia. (Sky Sports, via Mail)
Beki Mholanzi Pascal Struijk, 23, anasema anataka kusaini mkataba mpya na Leeds United. (Voetbalzone – in Dutch)
Chelsea imepata pigo katika jaribio lao la kumsajili mkuu wa zamani wa uhamisho wa Liverpool Michael Edwards miongoni mwa maafisa wake huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 43 akitaka muda wa kufikiria chaguo lake. (Sun)
Source: BBC SWAHILI