Kampuni ya Mawasiliano Tigo Tanzania imezindua rasmi Tigo Kili-Half Marathon 2023 ambayo itafanyika Mkoani Kilimanjaro ambako pia kuna Vivutio vya utalii ikiwemo mlima mrefu wa Kilimanjaro.
Meneja Mawasiliano wa Tigo Woinde Shisaeli alisema kwamba “Tunawakaribisha wote jioni hii katika hafla hii ya uzinduzi wa mbio za Kilimanjaro Marathon 2023 zitakazo fanyika mkoani Kilimanjaro,Mjini Moshi ambako ni mojawapo wa kitovu kikubwa cha shughuli za kiuchumi ikiwamo utalii kutokana na uwepo wa Mlima Kilimanjaro ambao ni mrefu kuliko yote barani Afrika” Woinde Shisaeli
Washiriki wa mbio hizo za #TigoKiliHalfMarathon2023 waahidiwa mazuri kwani wataweza kuwatumia marafiki, ndugu na jamaa, matukio mbali mbali matukio yatakayokuwa yanaendelea siku hio kupitia mtandao wetu ulioboreshwa kupitia mitandao ya kijamii kwa kutuma picha na video kupitia intaneti ya kasi ya 4G+