Kampuni ya Mawailiano TIGO Tanzania yafanya jitihada za kuunganisha shule za Sekondari katika mfumo wa Kidigitali. Jana ilifanikisha kuitembelea shule ya sekondari Chang’ombe, jijini Dar es salaam inayonufaika na mradi wake wa Tigo eSchools unaotekelezwa kwa ushirikiano na Nlab.
Kupitia mradi huo wa Tigo eSchools imeweza kuunganisha shule mbalimbali na Intaneti ya 4G+, kuweka mfumo wa maudhui kwa ajili ya wanafunzi kupitia tovuti ya www.tigoeschools.co.tz na kutoa mafunzo ya matumizi ya TEHAMA kwa walimu ili kurahisisha njia ya ufundishaji.
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT