Klabu ya Yanga SC, kwakushirikiana na UNICEF itatoa tiketi 10,000 kwa mashabiki wake watakaokubali kuelimishwa na kupatiwa chanjo ya Uviko 19 ndani ya siku 5 kuelekea mchezo wao wa mtoano wa kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya Club Africain.
–
“Ushirika wetu na UNICEF kuhusu Uviko-19 na virusi vya Ebola umeanza kazi rasmi ambapo tunatoa zawadi ya tiketi 10,000 kwa mashabiki ambao watachanja chanjo ya Uviko -19 kushuhudia mchezo wa Shirikisho Afrika dhidi ya Club Africain Novemba 2,” CEO wa Yanga, Andre Mtin.
–
Zoezi hilo litaanza Oktoba 29 hadi Novemba 2 na litafanyika katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam.