Homa ya Dabi ya Kariakoo Jumapili hii inaendelea kushika kasi kwa mashabiki pamoja na wadau mbalimbali wakitambiana mitaani na mitandaoni. Mwimbaji Tunda Man ambaye yeye ni shabiki wa klabu ya Simba akiwa pia ana nyimbo kadhaa za kuisifu klabu hiyo, ametoa ahadi kwa mashabiki wake kuelekea mtanange huo.
–
Kwenye mahojiano yake na EATV, Tunda Man amesema endapo klabu yake anayoishabikia (Simba) ikapoteza mchezo huo (ikafungwa na Yanga) basi ataacha kuimba nyimbo za Simba. Tunda Man amebainisha kuwa Simba inawachezaji wengi wazuri, bora na wanapambana.
–
“Kwa mchezaji mmoja mmoja sisi tunawachezaji wazuri kwa hiyo, kuhusu suala la timu nina timu nzuri na bora na inapambana. Sasa hivi nikifungwa tena na mtani siimbi tena nyimbo za Simba” – ameeleza Tunda Man akiiambia EATV.