Ripoti ya kuhuzunisha kutoka Afrika ya Kusini inaeleza ya kuwa Twiga amemuua mtoto mchanga wa miezi 16 katika mbuga ya wanyama huko Afrika Kusini.
–
Mtoto huyo na mama yake mwenye umri wa miaka 25 walikuwa katika mbuga hiyo kaskazini, KwaZulu-Natal muda ambao wote wawili walikua matatani kwa kukanyagwa na Twiga huyo.
–
Mtoto huyo alifariki baada ya kupelekwa katika zahanati iliyokuwa karibu kwa matibabu, huku mama yake akipelekwa hospitalini, akiwa katika hali mbaya, msemaji wa polisi aliviambia vyombo vya habari vya eneo hilo.
–
Ni nadra mno kwa twiga kuwashambulia wanadamu, hata hivyo uchunguzi unaendelea kujua ni kipi kilipelekea Twiga huyo kupata hasira na kuwakanyaga mama na mwanae.