Ujerumani imeweka wazi mpango wake wa kuhalalisha bangi, mabadiliko ambayo Waziri wa Afya wa nchi hiyo Karl Lauterbach amesema kuwa yanaweza yakawa mfano kwa Ulaya yote.
–
Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari jijini Berlin, Bw. Lauterbach ameeleza kuwa ”ikiwa sheria hii itapitishwa basi itakuwa ni mradi huria zaidi wa uhalalishwaji wa bangi barani Ulaya na hili litakuwa soko litakalodhibitiwa zaidi,” ”Utakuwa ni mfano utakaotumika na Ulaya.”
–
Katika mpango huo, itakuwa ni halali kabisa kwa watu wazima kununua na kuwa na bangi hadi gramu 30 kwa matumizi yao binafsi pia itaruhusiwa kuotesha mimea mitatu kwa kila kaya. Maduka yatakayokuwa na leseni yataruhusiwa kuuza bangi.
–
Waziri huyo amesema kuwa dhumuni kubwa ni kuwalinda vijana, ambao wengi wao tayari wanatumia bangi ambayo wanainunua kutoka kwenye masoko yasiyo rasmi.
–
Sambamba na mpango huo, serikali itaanzisha kodi ya matumizi ya bangi.