Kupata mimba ukiwa mkazi wa Kaunti ya Murang’a, huko Kenya kutakuingizia KShs. 6,000 ambayo ni zaidi ya shilingi laki moja za Tanzania (Tsh 115, 411) kutoka kwa mkuu wa Kaunti Mhe. Irungu Kang’ata.
–
Posho hii, anasema, italipwa kwa awamu tatu mwishoni mwa kipindi cha ujauzito.
–
“Tutakuwa tukiwasaidia akina mama wajawazito na malipo ya KSh. 2,000 kwa miezi miwili ya mwisho ya ujauzito wao na mara mbili ya kiasi hicho baada ya kujifungua, kufikia Ksh. 6,000 kwa kila ujauzito,” alisema.
–
Msaada huo wa kifedha unakusudiwa kuwafanya akina mama wajawazito kuwa na motisha na pia kusaidia kuongeza idadi ya watu wa eneo la Murang’as.
–
Baadhi ya watu wamekosea wakisema huenda hiyo ikachochea wanawake wengi wapate mimba kwa lengo la kujipatia pesa hiyo hata kama hana mpango wa kupata mtoto kwa kipindi hicho.