Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amesema Sheria ya Ustawi wa Jamii ikiundwa itarahisisha Uratibu wa utetezi wa haki za Makundi maalum.
Waziri Dkt. Gwajima ameyasema hayo wakati akifungua Mkutano wa mwaka wa Chama cha Maafisa Ustawi wa Jamii(TASWO) jijini Dodoma Oktoba 26, 2022.
Amesema Maafisa Ustawi wa Jamii hawajapata Sheria ya kitaaluma inayowezesha kufanya kazi kama madaktari wa Jamii hivyo kutokuwa na Baraza la Ithibati kwa watoa Huduma za Ustawi wa Jamii.
“Natambua kiu yenu ya kutaka Serikali ifanikishe uundwaji wa sheria ya taaluma yenu, mtakumbuka suala la sheria ya Ustawi wa Jamii ni mojawapo ya mambo tuliyoyapa kipaumbele kwani ikiwepo itarahisisha Uratibu wa utetezi wa haki za Makundi Maalum” amesema Dkt. Gwajima.
ADVERTISEMENT