Katibu wa UVCCM wilaya ya Temeke, Salum Dede, akipanda miti kwenye Zahanati ya Miburani. Leo Oktoba 14, 2022 Maadhimisho ya Miaka 23 kifo cha Baba wa Taifa, Mwl. Nyerere.
Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Miburani, Temeke, Dar es Salaam umeadhimisha Kumbukumbu ya miaka 23 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Julius Kambarage Nyerere kwa kufanya usafi, kupanda miti pamoja na kuchangia damu katika Zahanati ya Miburani.
–
Akizungumza mara baada ya zoezi hilo kukamilisha Katibu wa UVCCM wilaya ya Temeke, Salum Dede ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi, amewataka vijana kujifunza maisha ya baba wa Taifa Mwl.Nyerere kwa vitendo ili matendo ya kiongozi huyo wa kwanza wa Tanzania yaendelee kukumbukwa.
Katibu wa UVCCM wilaya ya Temeke, Salum Dede, akizungumza baada ya zoezi la usafi na kupanda miti kwenye Zahanati ya Miburani. Leo Oktoba 14, 2022 Maadhimisho ya Miaka 23 kifo cha Baba wa Taifa, Mwl. Nyerere.
“Ni miaka 23 sasa tangu kifo cha baba wa Taifa na Temeke sisi tuna Kata 23 ndiyo maana sisi tumelibaba kwa uzito jambo hili la kumuenzi Baba wa Taifa. Niwaombe sana vijana wa Temeke kutumia hazina ya wazee wetu na kuwa chachu ya kuishi kwa vitendo” alisema Dede Katibu wa UVCCM wilaya ya Temeke.
–
Naye Mtendaji Kata ya Miburani, Msiye Ngoi amewapongeza vijana hao wa UVCCM kata ya Miburani kwa kuona umuhimu wa kujitoa na kuwataka kuendelea kujitoa mara kwa mara. “Nawapongeza sana UVCCM Kata ya Miburani kwa kuona umuhimu wa kumuenzi baba wa Taifa kwa kufanya usafi, kupanda miti na kuchangia damu, ili ni Jambo la muhimu sana na tunawashukuru kwa moyo wenu huu wa kujitolea” amesema Ngoi.
Baadhi ya wachangiaji damu.
Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya Miburani, Keith Lupakisyo Mwambungu, amewashukuru vijana hao kwa kujitolea kufanya shughuli za kijamii kwa kufanya usafi na kuchangia damu katika Zahanati hiyo.
–
“Natoa Shukrani za dhati kwenu kwa niaba ya uongozi wa Zahanati ya Miburani kwa kuamua kujitolea kufanya shughuli za kijamii kwa kufanya usafi na kuchangia damu, Mungu awabariki kwa moyo huu” amesema Mwambungu.
Baadhi ya Viongozi na Waanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wakiga makofi kama ishara ya Pongezi wakati wa Zoezi la kupandaji miti kwenye Zahanati ya Miburani. Leo Oktoba 14, 2022. Maadhimisho ya Miaka 23 Kifo cha Baba wa Taifa, Mwl. Nyerere.
Diwani wa Kata ya Miburani, Mhe. Juma Rajabu Mkenga akipanda mti kwenye Zahanati ya Miburani, baada ya kufanya usafi katika Zahanati hiyo Leo Oktoba 14, 2022. Maadhimisho ya miaka 23 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Nyerere.
ADVERTISEMENT
Katibu wa UVCCM wilaya ya Temeke, Salum Dede pembeni yake Katibu wa UVCCM Kata ya Miburani, Mariam Ramadhani wakiwa katika zoezi la upandaji miti kwenye Zahanati ya Miburani, baada ya kufanya usafi katika Zahanati hiyo Leo Oktoba 14, 2022. Maadhimisho ya miaka 23 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Nyerere.
Katibu wa UVCC Kata ya Miburani, Mariam Ramadhani, akipanda mti katika moja ya eneo la Zahanati ya Miburani, baada ya kufanya usafi katika Zahanati hiyo Leo Oktoba 14, 2022. Maadhimisho ya miaka 23 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Nyerere. Katibu wa UVCCM wilaya ya Temeke, Salum Dede pembeni yake Katibu wa UVCCM Kata ya Miburani, Mariam Ramadhani wakiwa katika zoezi la upandaji miti kwenye Zahanati ya Miburani, baada ya kufanya usafi katika Zahanati hiyo Leo Oktoba 14, 2022. Maadhimisho ya miaka 23 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Nyerere.Baadhi ya Viongozi wa Jumuhia ya Wazazi na UWT na Waanachama wa Chama cha Mapinduzi (CCM) walioshiriki kwenye Zoezi la kupandaji miti kwenye Zahanati ya Miburani. Leo Oktoba 14, 2022. Maadhimisho ya Miaka 23 Kifo cha Baba wa Taifa, Mwl. Nyerere.
Baadhi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na UVCCM wakifurahia jambo baada ya kushiriki kwenye Zoezi la kupandaji miti kwenye Zahanati ya Miburani. Leo Oktoba 14, 2022. Maadhimisho ya Miaka 23 Kifo cha Baba wa Taifa, Mwl. Nyerere.
Baadhi ya wachangiaji damu.
Mwenyekiti wa UVCCM kata ya Miburani, Merry Materu akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya zoezi la usafi na upandaji miti kwenye Zahanati ya Miburani, kukamilisha, Leo Oktoba 14, 2022. Maadhimisho ya miaka 23 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Nyerere.
ADVERTISEMENT
Katibu wa CCM kata ya Miburani, Amir Matimbwa, akizungumza na Waandishi wa Habari baada ya zoezi la usafi na upandaji miti kwenye Zahanati ya Miburani, kukamilisha, Leo Oktoba 14, 2022. Maadhimisho ya miaka 23 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwl. Nyerere.