
Video ya wimbo wa Jugni ambao Diamond Platnumz ameshirikishwa na mwimbaji kutoka India, Diljit Dosanjh imefikisha watazamaji (views) Milioni 12 katika mtandao wa YouTube.
Video hiyo imefikisha watazamaji (views) ikiwa ni siku sita tu tangu ilipoachiwa rasmi YouTube kwenye Akaunti ya Diljit Dosanjh.
Wimbo huu ulipata views wengi zaidi ya milioni 1 ndani ya saa 8 tu baada ya kutolewa na zaidi ya views milioni 2 ndani ya masaa 13.
Ndani ya saa 14 video hiyo ilikuwa imekusanya views zaidi ya milioni 4 na kufikia zaidi ya milioni 5 ndani ya saa 18.
Mbali na kupata views wengi video hiyo pia imekuwa ikifanya vyema katika nchi kadhaa kama vile Kenya, Canada, Australia, New Zealand, Falme za Kiarabu , Uganda, na India.
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT