ADVERTISEMENT
Club Africain ni klabu iliyoanzishwa baada ya miaka 102 nyuma mwaka 1920 ndio ilianzishwa , Wakijulikana kwa jina maarufu “El Club” wanao uwanja unao ingiza mashabiki 60,000 uitwao Stade Olympique de Radès.
–
Club Africain ndio Klabu ya kwanza kutoka Tunisia kushinda “International Trophy” ambapo walishinda Maghreb Cup Winners mwaka 1971. . Baada ya miaka 20 , Mwaka 1991 Club Africain ikawa klabu ya kwanza kutoka Tunisia kushinda CAFCL kwa kipindi hicho iliitwa African Champions League.
–
Club Africain wamefanikiwa kutwaa makombe 13 ya ligi ya Tunisia na mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2015 , huku kombe la Tunisia Cup wakitwa mara 13 . Mara ya mwisho wakimfunga Ètoile de Sahel kwa magoli 4-1 mwaka 2018 na makombe matatu ya Tunisia Super Cup. . Larry Azounl ndio anatajwa kuwa mchezaji hatari kwenye kikosi hicho akiwa amesajiliwa €600 mwaka 2021 akiwa na miaka 28.

Larry alishawahi kuchezea timu ya vijana ya Ufaransa. . Kwenye hatua iliyopita ya Mashindano ya CAFCC Club Africain waliwatoa Klabu ya Kipanga kutoka Zanzibar kwa Aggregate ya magoli 7-0. . Kigingi kingine kwa Wananchi! Ni mda wa Yanga kuonesha ukubwa wao kwenye Mashindano ya Kimataifa.
Anaandika @kelvinrabson_
ADVERTISEMENT