
Walimu katika wilaya ya Mlele mkoani Katavi, wametakiwa kujiepusha na tabia ya kucheza michezo ya kubeti na kuchukua mikopo kandamizi ambayo imekuwa ikishusha heshima ya Mwalimu na utumishi wa umma.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Linkolin Tamba wakati wa mkutano mkuu wa Chama cha Waalimu wa mwaka.
Katibu Tawala ameenda mbali kwa kutoa mifano mbalimbali inayoharibu mipango ya walimu kupitia michezo ya bet ambayo ilipelekea mmoja wa mwalimu wa shule ya bweni kujikopesha fedha za wanafunzi wanazotumiwa na wazazi wao.
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT