Watu watatu katika kitengo cha wagonjwa wa kutengwa kwenye hospitali kuu nchini Uganda wamegunduliwa kuwa na virusi vya Ebola, Waziri wa afya nchini amethibitisha.
Katika ujumbe kwenye mtandao wa Twitter Waziri Jane Ruth Aceng ameeleza kwamba watu watatu miongoni mwa watu 60 katika kitengo cha wagonjwa wa kutengwa Mulago Oktoba 21 walipatikana na Ebola
Waziri huyo wa afya ameeleza kwamba watahamishwa hadi Entebbe kupata matibabu kwasababu kituo cha Mulago bado kina watu 58 ambao wapo kwenye karantini.
Uthibitisho wa visa hivyo vya Mulago unatokea siku ambayo pia wizara ya habari imeeleza kwamba mlipuko wa Ebola nchini humo unadhibitiwa na unatarajiwa kumalizika kufikia mwishoni mwa mwaka.