Madaktari Bingwa kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakishirikiana na Madaktari Bingwa wa Taasisi ya Mending Kids ya Marekani katika kufanya upasuaji wa bila kufungua kifua kwa watoto 40 wenye matatizo ya moyo.
Utaratibu wa upasuaji ya watoto hao, ilianza Oktoba 17 na kuhitimishwa leo Oktoba 21 ambapo upasuaji wa watoto 20 ulihusisha kufungua kifua na wengine 20 matibabu kwa njia ya tundu dogo.
Hayo yameelezwa leo Oktoba 21 Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI, Dk Peter Kisenge kwenye mkutano na waandishi wa habari akizungumzia mafanikio ya kambi ya madaktari hao kwenye taasisi hiyo.