Mamlaka za usalama nchini Pakistan zimesema kuwa watu 18 wakiwemo watoto 12 wamefariki baada ya basi waliyokuwa wakisafiria kuteketea kwa moto kutokana na hitilafu ya mfumo wa umeme.
–
Afisa wa polisi wa eneo hilo Javed Baloch amesema basi hilo lilikuwa limewabeba watu 50 wenye uhusiano wa kindugu wakitokea mji wa kusini wa Karachi kuelekea Jimbo la Sindh .
ADVERTISEMENT
–
ADVERTISEMENT
Watu hao walihamia Karachi mwezi Agosti baada ya mji wao wa Khairpur Nathan Shah kukumbwa na mafuriko makubwa yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 2,000 nchini humo.