Waziri mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika Ziara yake mkoani Mwanza akiambatana na Mkuu wa mkoa hua Mh. Adam Malima amepata nafasi ya kutembelea Stendi ya Zamani ya Mabasi ambayo ilisitishwa kutoa huduma kwa muda ili kupisha zoezi la Ujenzi wa kituo bora kitachokizi huduma na idadi kubwa ya Wanaosafiri wakati wowote. Stendi hio imekamilika kwa kiwango kikubwa kuelekea kuanza rasmi kutumika siku chache zijazo baada ya kuweka Utaratibu maalum wa namna ya Uendeshaji.
Waziri Mkuu Majaliwa ameeleza kwamba stendi hio itumike na Mabasi ya Mikoani kama vile yatokayo Dar es Salaam, Ifakara, na sehemu nyingine za mkoa.