Xi Jinping amechaguliwa tena kuwa katibu wa chama kwa muhula wa tatu mfululizo.
–
Xi Jinping amehutubia vyombo vya habari, akisema kwamba chama jana kilimaliza kwa mafanikio kongamano lake, kwa ‘’kushikilia bendera yetu, kuunganisha nguvu zetu na kusonga mbele kwa umoja’’.
–
Pia alibainisha kuwa jumuiya ya kimataifa imekuwa ikifuatilia kongamano hilo ‘’kwa shauku kubwa’’ na wakuu wa nchi wametuma salamu za pongezi na barua, na aliwashukuru wote.
–
Kisha akatambulisha safu yake mpya katika kamati ya kudumu ya chama, na kuongeza ‘’wote wanajulikana kwenu’’.
–
Xi, 69, ndiye kiongozi wa chama mwenye nguvu zaidi tangu kiongozi wa kwanza wa zama za kikomunisti Mao Zedong aliyefariki mwaka 1976.
–
Xi anaendelea na cheo cha kiongozi wa kijeshi kama ilivyotarajiwa
–
Imetangazwa kuwa Xi pia ataendelea kuwa Mwenyekiti wa Tume Kuu ya Kijeshi – kumaanisha kuwa yeye ndiye kamanda anayesimamia Jeshi la Ukombozi la Watu wa China.
–
Hiyo ina maana kwamba Xi tena ni katibu wa chama, kamanda wa kijeshi na kwa hakika atakuwa pia rais wa China (mkuu wa nchi ambaye anahitaji tu uthibitisho wa kiufundi katika kura ya wabunge mapema mwaka ujao).