MABINGWA watetezi, Yanga SC wametoa sare ya kufungana bao 1-1 na Simba SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
ADVERTISEMENT
–
Simba ndiyo walikuwa wa kwanza kufunga bao dakika ya 14′ kupitia kwa Augustine Okrah na baadae dakika mbili kabla ya kwenda mapumziko Aziz Ki alisawazishia Yanga kwa shoti kali la adhabu ndogo lilomshinda Mlinda Mlango, Aish Manula.
ADVERTISEMENT