
Staa kutoka lebo ya WCB Wasafi, Zuchu ametajwa kuwania tuzo za kimataifa za MTV EMA kwa mwaka huu katika kipengele cha msanii bora wa Afrika.
Katika kipengele hicho, Zuchu anashindana na wasanii wengine Burna Boy , Tems, Ayra Starr, Black Sherif wa Ghana na Musa Keys
Zuchu ndiye msanii pekee kutoka Afrika Mashariki katika tuzo hizo, akiingia akiwa na kumbukumbu za ushindi wa Bosi wake Diamond Platnumz alioupata katika kipengele hicho mwaka 2015, pamoja na Ali Kiba aliyefanya hivyo mwaka 2017.