Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa ametoa ripoti ya awali ya uchunguzi wa ajali ya ndege ya Precision iliyoua Watu 19 Bukoba.
Waziri Mbalawa alifunguka yafuatayo kulingana na utaratibu wa kutoa ripoti ya awali kuhusu ajali ya ndege kwa sababu hapo siku chache nyuma kulikuwepo na ripoti inayosambazwa pasipo kutoka katika chanzo chenye dhamana hio;
“Mwenye dhamana ya kutoa ripoti ni mimi kwa sababu mimi ndiye Waziri ninayesimamia usafiri wa anga, hivyo mimi leo ndiyo ninatoa ripoti, wewe unaweza kutoa ripoti yako kama utaona inafaa lakini mwenye mamlaka ni Waziri mwenyewe,”- Profesa Makame Mbarawa