Watu saba (7) wamefariki dunia na wengine sita kujeruhiwa baada ya gari la wagonjwa (Ambulance) na Prado kugongana uso kwa uso katika eneo la Pori namba Moja huko wilayani Kiteto mkoani Manyara
–
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mkuu wa wilaya ya Kiteto Mubaraka Batenga Amesema kuwa Gari la wagonjwa kutoka kituo cha Sunya lilikua linatokea Kibaya kupeleka mgonjwa na baada ya Kumshusha mgonjwa likawa linarejea kwenye kituo chake lakini Bahati mbaya likagongana uso kwa uso na Prado ambalo lilikua linatokea upande wa Kilindi kuelekea Kibaya
–
Majeruhi wanne wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Benjamin Mkapa Dodoma huku wawili wakiendelea kupewa matibabu katika Hospitali ya wilaya ya Kiteto mkoani Manyara
–
DC Batenga amemaliza kwa kusema kuwa waliofariki kwenye ajali hiyo walikua kwenye gari la Wagonjwa (Ambulance huku sita walifariki papo hapo na mmoja amefariki akiwa anapatiwa matibabu