Kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa Didier Deschamp amesema kuwa ni pigo kwa kikosi chake kumkosa Karim Bemzema kwa sababu ya kuwa majeruhi.
–
” Ninasikitika sana kwa kutokuwepo kwake, lakini bado nina matumaini tutafanya vizuri. Tupo tayari kukumbana na changamoto hizi,” amesema
–
Shirikisho la soka la Ufaransa ( FFF) lilithibitisha kutokuwepo kwa Benzema kikosini baada ya kufanyiwa kipimo cha MRI katika hospital ya mjini Doha na kukutwa na matatizo katika sehemu yake ya paja.
–
Tangu aliposhinda taji la Ballon D’or mwezi uliopita, Benzema hajaichezea Real Madrid kwa zaidi ya nusu saa wakati wa mechi ya Ligi ya mabingwa dhidi ya Celtic. Benzema ana umuhimu mkubwa sana katika kikosi hicho cha Ufaransa.
–
Alikuwa mfungaji anayeongoza katika michuano ya kombe la dunia ya mwaka 2014, lakini hakuwepo katika kikosi cha kombe la dunia cha mwaka 2018 ambalo Ufaransa ilishinda taji.
–
Kocha wake Deschamp alimwita tena kikosini baada ya kuwa mfungaji bora.
–
Kikosi hicho cha Ufaransa, mbali na Benzema, pia kitawakosa Paul Pogba na N’ Golo Kante ambao walikuwepo katika kikosi kilichoshinda taji la kombe la dunia.