Kipa wa zamani wa klabu ya Manchester United Anders Lindegaard (38) ametangaza kustaafu soka.
–
Tangazo hilo limekuja mara baada ya kutangazwa kwa kikosi cha Denmark kitakachoenda kwenye kombe la dunia ambapo kipa huyo hakuwemo. Nyota huyo hajaichezea timu yake ya Taifa tangu mwaka 2011.
–
ADVERTISEMENT
Kupitia mtandao wa Instagram Lindegaard ameandika ujumbe wenye hisia kubwa na kusema anashukuru kwa kumbukumbu zote ndani ya miaka yake 20 katika soka.
–
Alijiunga na Manchester United mwezi Januari mwaka 2011 na kuondoka mwaka 2015 katikati.