ADVERTISEMENT
Timu ya Wanawake ya Arsenal Women imeweka rekodi ya kushinda mechi 14 mfululizo za Ligi Kuu ya Wanawake England. Wamefikisha idadi hiyo baada ya usiku wa jana kuifunga Leicester Women mabao 4-0.
–
Mabao yaliofungwa Frida Leonhardsen-Maanum dakika ya 13′, Caitlin Foord dakika ya 22′, Stephanie Catley dakika 37 pamoja na Stina Blackstenius dakika ya 48′.
–
Arsenal Women ndio vinara wa Ligi Kuu ya Wanawake England wakiwa na alama 18 sawa na Chelsea Women walipo nafasi ya pili, tofauti yao mabao ya kufunga na kufungwa.
–
Chelsea Women wao wakicheza mechi 7, wakipata ushindi mechi 6 na kupoteza mechi 1, wakifunga mabao 17 na kufungwa mabao 6 huku Arsenal Women wao wakiwa wamecheza mechi 6 wakipata ushindi mechi zote 6, wakifunga mabao 18 na kuruhusu kufungwa bao moja tu.
ADVERTISEMENT