Kocha mkuu wa Arsenal, Mikel Arteta amesema kwa mwendo wa kikosi chake sasa ni wazi kuwa wapo katika mbio za kuwania ubingwa wa ligi kuu ya England msimu huu.
–
Arteta ametoa kauli hiyo mara baada ya kushuhudia vijana wake wakiisambaratisha Chelsea kwa bao moja kwa sifuri katika dimba la Stanford Bridge.
–
Tangu kuanza kwa msimu huu, Arteta alikuwa kimya kuhusiana na nia ya kikosi chake ya kuwania ubingwa wa EPL msimu huu, lakini sasa ameanza kuona mwanga kuelekea katika ubingwa.
–
Akizungumza wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari Arteta amesema licha ya kuwa kileleni kwa tofauti ya alama mbili dhidi ya Manchester City lakini matumaini ya kutwaa ubingwa msimu huu yameanza kuonekana.
–
“Inabidi tuwe waangalifu na heshima kubwa kwani timu tunayoshindana nayo kwa sasa ni nzuri na inapata matokeo kila wakati na hii haitakuwa rahisi.” amesemaM Arteta.