ADVERTISEMENT
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv
Tuesday, September 26, 2023
  • Login
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
  • Home
  • HABARI
  • BURUDANI
  • BIASHARA
  • MICHEZO
  • MAGAZETI
  • MAGAZETI TANZANIA
  • KIMATAIFA
  • KONCEPT TV
No Result
View All Result
Mwanaharakati Mzalendo
No Result
View All Result

ASILIMIA 70 YA MAGONJWA YA MILIPUKO HUTOKANA NA UCHAFU

Dodoma, Tanzania

MTEWELE ALFRED by MTEWELE ALFRED
Nov 17, 2022
in HABARI
0
ASILIMIA 70 YA MAGONJWA YA MILIPUKO HUTOKANA NA UCHAFU
0
SHARES
74
VIEWS
Share on FacebookShare on Twitter

RelatedPosts

WATU 128 WAPATA HUDUMA YA KUPUNGUZA UZITO ULIOPITILIZA

WATU 128 WAPATA HUDUMA YA KUPUNGUZA UZITO ULIOPITILIZA

Aug 2, 2023

FAIDA ZA ULAJI WA PARACHICHI KIAFYA

Aug 1, 2023

MUHIMBILI YAKIDHI VIGEZO KUSHUGHULIKIA DHARURA AFCON 2027

Aug 1, 2023
Load More

May be an image of 7 people, people standing and outdoorsImeelezwa kuwa udhibiti wa usafi binafsi na wa mazingira unasaidia kupunguza asilimia 70 ya magonjwa ya milipuko yanayotokana na uchafu ikiwemo Kipindupindu.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Kinga Dkt. Beatrice Mutayoba mara baada ya kufanya usafi kwenye soko la Bonanza lililopo kata ya Chamwino jijini Dodoma ikiwa ni kuelekea wiki ya usafi wa mazingira na matumizi ya choo yanayofanyika kila mwaka Novemba 15-19.
“Usafi wa mazingira unasaidia kupunguza asilimia 70 ya magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu hivyo maofisa afya na watendaji wa kata mnapaswa kusimamia vizuri usafi wa mazingira mita tano (5) kuzunguka maeneo ya watu wanayofanyia kazi, ofisini, mashuleni na kwenye nyumba zao ili kuepuka magonjwa ya mlipuko yanayosababishwa na uchafu.” Amesema Dkt. Mutayoba
Aidha, amesema kufanya usafi kwenye mazingira ya kuishi ni jambo jema na kitu kinachosaidia kudhibiti uchafuzi wa vyanzo vya maji chini ya ardhi pamoja na kudhibiti magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu pamoja na magonjwa mengine yanayosababishwa na uchafu.
Dkt. Mutayoba ameongeza kuwa kila eneo lina mwenyewe hivyo ni vyema kusimamia vizuri ili hata usafi wa mwisho wa mwezi au kila jumamosi itatusaidia kupunguza kuharibu mazingira.
“Ni vyema sasa kuweka usimamizi kwenye maeneo ya soko ili kuepuka magonjwa ya mlipuko kama kipundupindu pamoja na kusafisha mitaro ya majitaka.” Amesema Dkt. Mutayoba
Hata hivyo Dkt. Mutayoba amewataka maofisa afya pamoja na viongozi wa mitaa na kata kusimamia ujenzi wa miundombinu ikiwemo ujenzi wa vyoo bora na kuvitumia kwa kuweka miundombinu ya kunawia mikono pamoja na kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu usafi wa mazingira na usafi binafsi.
Wakati huo huo Dkt. Mutayoba amewataka maofisa afya kusimamia sheria na kanuni za usafi wa mazingira ili kuwadhibiti wale wote wanaojenga kwa kuziba mitaro ya maji kwenye maeneo ya masoko ili kuepuka magonjwa ya milipuko watati wa mvua.
Naye, Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Prof. Davis Mwamfupe amewataka wafanya biashara hadi jumamosi wiki hii wale wote walioweka makaravati kwenye mitaro kuvunja mara moja na kujenga vidaraja ambavyo watatumia kupitisha takataka chini ili kuepusha magonjwa ya mlipuko hususan wanapoelekea msimu wa mvua.
Amesema kuwa inahitajika uhamasishaji kwa wananchi ili waelewe kwamba usafi ni tabia ya mtu, kujisikia mahali alipo si sehemu salama au pachafu hivyo kujenga tabia ya usafi wote na kupelekea kutoa wito kwa maofisa Afya kuendelea kutoa elimu hiyo kwa wananchi wote.
Amesema halmashauri ya jiji imeingia mkataba na kampuni kutoka Zimbabwe kwa lengo la kuchakata taka kutoka kwenye dampo la halmashauri hiyo ambapo taka hizo zitakua fursa kwa wakazi hao ya kuwapatia mbolea na gesi.
May be an image of 5 people and people standing

Related

Tags: Wizara ya Afya
MTEWELE ALFRED

MTEWELE ALFRED

Related Posts

MKURUGENZI MPYA TANESCO APEWA MIEZI SITA TATIZO LA UMEME
HABARI

MKURUGENZI MPYA TANESCO APEWA MIEZI SITA TATIZO LA UMEME

by SUZO SHUKRANI
Sep 26, 2023
ESWATINI KUFANYA UCHAGUZI WA WABUNGE
HABARI

ESWATINI KUFANYA UCHAGUZI WA WABUNGE

by SUZO SHUKRANI
Sep 26, 2023
MKUU WA WILAYA YA KINONDONI, MH. SAADI MTAMBULE AZINDUA KITUO CHA MFUMO WA M-MAMA JIJINI DAR ES SALAAM.
HABARI

MKUU WA WILAYA YA KINONDONI, MH. SAADI MTAMBULE AZINDUA KITUO CHA MFUMO WA M-MAMA JIJINI DAR ES SALAAM.

by I am Krantz
Sep 26, 2023
WAPATA UMEME KWA MARA YA KWANZA TANGU NCHI IPATE UHURU
HABARI

WAPATA UMEME KWA MARA YA KWANZA TANGU NCHI IPATE UHURU

by SUZO SHUKRANI
Sep 26, 2023
WAZIRI AWESO HATUWEZI KUFANYA KAZI PEKE YETU
HABARI

WAZIRI AWESO HATUWEZI KUFANYA KAZI PEKE YETU

by SUZO SHUKRANI
Sep 26, 2023
TAMISEMI YATOLEA UFAFANUZI SAKATA LA DADA WA KAZI KUKOSA MASOMO
HABARI

TAMISEMI YATOLEA UFAFANUZI SAKATA LA DADA WA KAZI KUKOSA MASOMO

by SUZO SHUKRANI
Sep 26, 2023

KRANTZ MWANTEPELE (FOUNDER & CEO)

KONCEPT TV

https://www.youtube.com/watch?v=0HP0mB_rtIU&t=7s
KONCEPT TV

KONCEPT TWEETS

November 2022
M T W T F S S
 123456
78910111213
14151617181920
21222324252627
282930  
« Oct   Dec »
Currently Playing
  • About
  • Advertise
  • Privacy & Policy
  • Contact

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

No Result
View All Result
  • Home
  • Habari
  • Biashara
  • Afya
  • Kisamkasa
  • Magazeti
  • Makala
  • Michezo
  • Teknolojia
  • Koncept Tv

All rights reserved © 2020 Mwanaharakati Mzalendo - Powered by Koncept.

Welcome Back!

Login to your account below

Forgotten Password?

Retrieve your password

Please enter your username or email address to reset your password.

Log In