ADVERTISEMENT
Mchezaji wa klabu ya Simba, Peter Banda amefunguka kukosekana Uwanjani kwa takribani miezi 3, hiyo ni kutokana na matokeo ya majeraha ambayo aliyapata wakati wa mchezo wao dhidi ya Singida Big Stars FC uliochezwa katika uwanja wa LITI Mkoani Singida, ambapo ndie pia mchezaji pekee aliyeweza kusawazisha goli na kufanya klabu yake kutoa Sare ya 1-1 dhidi ya mpinzani wake.
@peterbanda amefunguka yafuatayo “Habari zenu watu wema 👋🏾 habari za leo? Ninajisikia vizuri sasa kuliko hapo awali. Nitaenda kumuona daktari baada ya wiki mbili tena kwa uchunguzi lakini kulingana na matokeo, nitakuwa nje kwa miezi mitatu. Natumai, kwa neema ya Mungu, nitarudi uwanjani mnamo Februari”.
…………”Hello good people
how are you today ?I am feeling better now than before. I will go see a doctor after two weeks again for a checkup but according to the results, I will be out for three months. Hopefully, by God’s grace, I will be back on the field in February”.



ADVERTISEMENT