ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT
Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya CRDB, Toyi Ruvumbangu ameendesha kikao cha maandalizi ya safari ya wafanyabiashara kuelekea nchini India
katika Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara yanayofanyika nchini humo kuanzia tarehe 16 hadi 21, safari iliyoandaliwa na Benki kwa kushirikiana na kampuni ya GoExtra Mile.

Ruvumbangu amesema Benki ya CRDB inatambua umuhimu wa sekta ya biashara katika kuchochea uchumi na ndiomana imekuwa ikiweka jitihada kubwa katika kuwawezesha wafanyabiashara kujifunza kutoka katika mataifa yaliyoendelea.
Kwa upande wao wafanyabiashara wameishukuru Benki ya CRDB kwa kuendelea kufadhili safari za mafunzo nje ya nchi wakibainisha kuwa zimekuwa msaada mkubwa katika kuboresha biashara zao kuendana na mahitaji yaliyopo.
Katika safari hiyo wafanyabiashara watatembelea katika miji mitatu mikubwa nchini India ya Delhi, Mumbai, na Punjab.
