
Benki ya CRDB imefungua rasmi tawi jingine jipya la Ludewa mkoani Njombe. Tukio hilo liliongozwa na Katibu Tawala wa Wilaya ndugu Daniel Ngalupela kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ludewa.
Hafla ya uzinduzi wa tawi imehudhuriwa na viongozi pamoja na wafanyakazi wa Benki ya CRDB, viongozi wa wilaya ya Ludewa wakiongozwa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa ndugu Deogratius Sunday, Mbunge wa Jimbo la Ludewa Mh Joseph Kamonga, Viongozi wa Dini na Wateja wa benki ya CRDB.


ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT