Benki ya CRDB imeshiriki Kongamano la 26 la Tafiti lilioandaliwa kwa ushirikiano na Taasisi ya Utafiti ya REPOA na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Kongamano hilo ambalo limepewa kauli mbiu ya “Uhuishaji wa Biashara na Mabadiliko ya Tabianchi Uchumi shindani wa Kijani” lilizinduliwa na Rais wa Zanzibar, Mhe. Dkt. Hussein Ally Mwinyi.
Akizungumza katika kongamano hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema Benki imejidhatiti katika ufadhili wa miradi ya kijani katika sekta mbalimbali ikiwamo biashara na kilimo.
Nsekela alisema kupitia usahili wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabiachi (GCF) benki inaweza kutoa ufadhili wa hadi USD 250 Milioni kwa mradi mmoja.
Aidha alibainisha kuwa benki ipo katika hatua za mwisho kuanzisha program ya ufadhili wa miradi ya kilimo stahimilivu kupitia teknolojia (TACATDP) ambapo jumla ya USD 200 milioni zimetengwa.
Wadau kutoka sekta mbalimbali za maendeleo ndani na nje ya nchi
wamehidhuria kongamano hilo linalofanyika katika hoteli ya GoldenTulip Zanzibar.