
Benki ya CRDB imezindua App ya CRDB Bank Wakala, Inayomuwezesha wakala kuwahudumia wateja kiurahisi, kwa uhakika na salama zaidi.
Kupitia App hio Wakala hana stress za mtandao kukwama, atawapatia huduma muda wowote mahali popote, yaani anakufanikishia miamala yako kwenye dunia ya kisasa.
Hafla ya Uzinduzi iliongozwa na mgeni rasmi Waziri wa Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mh. Nape Nauye Ikihudhuriwa na Mkurugenzi mtendaji wa benki ya CRDB Bw. Abdulmajid Nsekela, Wakurugenzi, wafanyakazi wa CRDB pamoja na Mawakala mbalimbali.

” Kuanzishwa kwa huduma za kifedha kwa njia ya simu, pamoja na huduma za benki kwa wakala, kumeongeza upatikanaji wa huduma za kifedha nchini hususan maeneo ya vijijini, na kupunguza gharama za miamala ya kifedha.” – Abdulmajid Nsekela


ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT