ADVERTISEMENT

Benki ya NBC kwa kushirikiana na Jubilee Insurance, imetoa mafunzo kwa mashirika zaidi ya 100 ya bima ili kuimarisha upatikanaji wa huduma hiyo nchi nzima. Benki hio inafanya hivyo ikiwa kama sehemu ya juhudi zake za kuimarisha huduma za bima nchini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo ya siku 4 kwa mashirika ya bima jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi, alisema Benki ya NBC imeanza mpango mkakati wa kuhakikisha matumizi kamili ya teknolojia na mifumo ya kidijitali yanaendelea kuwa sehemu muhimu katika utoaji wa huduma za Benki ya NBC.
“Ili kuhakikisha benki inatoa huduma bora za bima, tumeanza mpango mkakati utakaohakikisha matumizi ya teknolojia na mifumo ya kibenki ya kidijitali inaendelea kuwa sehemu muhimu ya utoaji wa huduma zetu za benki ili kuongeza upatikanaji wa huduma hii nchini nzima. ,” alisema Bw. Sabi.



ADVERTISEMENT