ADVERTISEMENT
Benki ya NMB ikiwa Kama mdau wa Sekta ya Ujenzi nchini, imeandaa warsha iliyowakutanisha wadau wa Sekta ya Ujenzi Zanzibar ili kutambulisha suluhishi zake mbalimbali zinazolenga kuboresha utekelezaji wa miradi yao.
Warsha hii imehudhuriwa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi wa Serikali ya Mapinduzi – Zanzibar, Dkt. Khalid Salum Mohamed; Waziri wa Ardhi wa Serikali ya Mapinduzi – Zanzibar, Mhe. Rahma Kassim Ali, pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi wa Serikali ya Mapinduzi – Zanzibar, Mhe. Juma Makungu Juma. Benki hio imewakilishwa na Mkuu wa Idara ya Miamala ya Benki, Bi. Linda Teggisa pamoja na Meneja wa Biashara Zanzibar, Bi. Naima Shaame.
ADVERTISEMENT