Mkurugenzi mtendaji wa Benki ya NMB Bi. Ruth Zaipuna ameshiriki maonyesho ya tuzo 18 za kitaifa na kimataifa ambazo ilizozipata mwaka huu zinazotambua ubora wa benki hio katika utoaji huduma kwa wateja, wadau na watanzania kwa ujumla. Benki hio @nmbbank_tz imeandika…..”Sio Moja Wala Mbili, ni18!”
Baadhi ya tuzo ilizozitangaza leo kutoka kwenye majarida ya kimataifa ni:
Benki Bora Tanzania kwa mwaka 2022 – Kutoka Jarida la Global Brands Magazine
Benki Bora ya Wateja Binafsi na Biashara – Kutoka Jarida la World Economic Magazine, Jarida la International Business Magazine na Jarida la Global Banking and Finance Review
Benki Bora katika Kilimo Biashara – Kutoka Jarida la Global Brands Magazine
Ubunifu Bora katika Huduma za Kibenki kwa Wateja Binafsi Tanzania – Kutoka International Bankers Award
Benki Bora kwa Wateja Maalum – kutoka International Bankers
Afisa Mtendaji Mkuu Bora kwa Mabenki nchini Tanzania – kutoka Jarida la World Economic Magazine, Jarida la Global Brands Magazine na African Bank 4.0 Summit
Hatifungani Bora ya Mwaka 2022 – kutoka Mtandao wa Mitaji kwa Wajasiliamali Wadogo na wa Kati ambao wameshirikiana na nchi za G20 na IFC.
Imewashukuru wateja wake, wadau pamoja na Watanzania wote kwa kuendelea kushirikiana nao na kuongeza kuwa Mafanikio hayo ni ya wote kwa pamoja!
Related