Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dk. Dorothy Gwajima @gwajimad amekutana na Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania Mhe. Mantredo Fanti ambaye, wamekubaliana kuendelea kushirikiana katika Programu ya kutokomeza Ukatili wa kijinsia na uwezeshaji Wanawake kiuchumi, ambapo Balozi huyo amebainisha kuwa Umoja wa Ulaya umetenga jumla ya ‘Euro’ milioni 70 sawa na shilingi za Kitanzania Bil 169.14, kwa ajili ya Programu hizo.
ADVERTISEMENT
ADVERTISEMENT