Fundi bomba aliyekuwa anatengeneza katika nyumba moja huko Edinburg hakuamini macho yake alipokutana na chupa iliyofukiwa chini ya sakafu kwa miaka 135.
–
Fundi huyo, Peter Allan aliikuta chupa hiyo chini ya sakafu wakati akiwa katika ujenzi wake. Alikimbia kwenda kumtaarifu mteja wake juu ya chupa hiyo. Anasema hakuamini macho yake baada ya kuchimba chini umbali mrefu na kuikuta chupa hiyo ikiwa na karatasi ndani yake.
–
” Niliichukua na kumuonyesha mwenye nyumba nilichokiona,” amesema fundi huyo.
–
Mteja huyo, Eilith Stimpston alipoivunja alikuta ujumbe ndani yake uliohifadhiwa ndani ya chupa hiyo kwa miaka 135. Inasemekana kuwa chupa hiyo ilifukiwa ndani ya chumba cha nyumba hiyo wakati ilipojengwa.
–
Mwenye nyumba huyo ambaye anaishi na mume wake alisubiri hadi watoto wake wawili walipotoka shule na kuvunja kujua ujumbe gani uliopo ndani yake. Lakini anasema aliogopa kuvunja chupa hiyo yenye miaka 135, lakini ilimbidi afanye hivyo ili kujua kuna ujumbe gani ndani yake.
–
Waliporudi alichukua nyundo na kuivunja . Walikuta ujumbe ulioandikwa na mafundi wawili wa kiume ambao waliandika kifuatacho.
–
” James Ritchie na John Grieve ndio waliotengeneza msingi wa nyumba hii Oktoba 6, 1887, lakini hawakupewa whisky,”.