Programu maalum ya CHIPSIKA KIAJIRA NA COKE iliyoandaliwa na Kampuni ya Cocacola kwanza iliyopo jijini Dar es Salaam imeleta tija kwa wafanyabiashara wa Chipsi waliopo mtaani jijini humo kwa kuwapatia vifaa ambavyo ni jiko kubwa la gesi lenye sahani mbili, mtungi wa gesi mmoja, na mavazi wezeshi, vitakavyowawezesha kuhudumia idadi ya wateja wengi kwa muda mfupi.
Yafuatayo yalielezwa kama sehemu ya Kampuni kujivunia na Programu hio “Tunayofuraha kuwashirikisha kuwa tumezindua rasmi programu yetu ya ujumuishaji wa vijana kiuchumi iitwayo “Chipsika Kiajira na Coke” yenye lengo la kusaidia zaidi ya watu 900 wanaojishughulisha na biashara maarufu ya chipsi katika mitaa ya Dar es Salaam. Kwa ubia na ISW na M-gas tutawapa zana za biashara na ujuzi muhimu ili kukuza biashara zao”.
#chipsikakiajiranacoke